KARIBU KATIKA JUKWAA LA KISWAHILI...MOHAMMED SAID MOHAMMED...+255 777 05 14 54 / +255 773 558 812/ +255 657 509 114.. MSINGINI MKOANI PEMBA...AHSANTENI
:::Advertise with us to make your business or program visible in all East African countries and the rest of the world - JUKWAA LA KISWAHILI.:::

Sunday, March 29, 2015

TAALUMA YA ISIMU

Wapenzi wanafunzi wa vyuoni ,karibuni katika somo letu la leo katika muendelezo wa kukitangaza na kukikuza kiswahili Tanzania na duniani kwa ujumla.Changi maoni yako.
           
  MUKHTASARI WA DHANA YA TAALUMA YA ISIMU

Wanaisimu wengi wamejaribu kufasili dhana ya isimu .kwa mfano  , Richards et al (1985) anasema kuwa :

Isimu ni mtalaa ambao huchunguza lugha kama mfumo wa mawasiliano ya mwanaadam (TY)
Hartman (1972) naye anasema:
Isimu ni eneo maalum la mtalaa ambalo lengo lake huwa ni kuchunguza lugha .Wanaisimu huzichunguza lugha zikiwa ni nyenzo muhimu za mawasiliano ya mwanaadamu. (TY).
Verma et al (1989)wanasema kuwa isimu ni sayansi kwa sababu hufuata mbinu za kimsingi za utafiti wa kisayansi.Mbinu hizi huhusisha sifa zifuatazo.
1. Uchunguzi uliodhibitiwa
2. Uundaji wa haipothesia
3. Uchanganuzi
4. Ujumlishi
5.Utabiri
6.Majaribio na uthibitishaji
7. urekebishaji au ukataaji wa haipothesia
Hii ni kusema kuwa isimu haichunguzi lugha kiholela bali kwa uratibu na mwelekeo maalumu.katika kuchunguza lugha ,wanaisimu hutumia misingi ya kisayansi kama zifanyavyo sayansi zingine.

 TUKI (1990)  wanasema kwa ufupi kabisa sana
Isimu ni sayansi ya lugha.

MATAWI YA SAYANSI
Isimu historia
Isimu fafanuzi
Isimu linganishi
isimu jamii
isimu tumizi
isimu nafsia.

USAYANSI WA ISIMU
 Utoshelevu wa kiuteuzi
Utoshelevu wa kiuchunguzi
utoshelevu wa kiufafanuzi
Uchechevu
Uwazi

 MISINGI YA USAYANSI WA ISIMU
Uwazi
Utaratibu
Urazini

MAREJEO
Mgullu,R.S. (1999) Mtalaa wa Isimu Fonetiki,Fonolojia na Mofonolojia ya Kiswahili.Longhorn    Publishers:Dar es salaam,Tanzania.
Habwe,J. na wenzake (2004) Misingi ya sarufi ya kiswahiliPhoenix Publishers :Nairobi,Kenya.

13 comments:

  1. Misingi ya usayansi wa lugha haijitoshelezi

    ReplyDelete
  2. Mbona hakuna mpangilio mwnzo hadi mwisho??

    ReplyDelete
  3. Mumejitshidi kwa kiasi lkn bado kidogo

    ReplyDelete
  4. Samahani taaluma za isimu ni zipi??

    ReplyDelete
  5. Samahani taaluma za isimu ni zipi??

    ReplyDelete
  6. Kwa kiasi Fulani, kueleza isimu ni sayansi mmetoa wanga kwa wasomaji

    ReplyDelete
  7. Mchango wa wahindi na roma kuendeleza Isimu ni upi?

    ReplyDelete
  8. Ni yapi matawi ya isimu fafanuzi?

    ReplyDelete
  9. Misingi ya usayansi wa lugha haijafafanunuliwa zaidi

    ReplyDelete
  10. Kwann isimu Ni sayansi ya lugha

    ReplyDelete