Mtunzi na Mhariri wa makala hii ni Ndugu,Mohammed Said .
Awali ya yote,tunatanguliza salamu kwa kutakiana upendo na amani .Lengo la makala hii ni kuwahamasisha wanajamii hata kawa mfano wa vidole katika miili yetu; kwani kila kiungo kimoja katika miili yetu, kinahitaji&kutegemea kiungo kingine kukamilishana na kusaidiana.Tujiulize nani rafiki na yupi anafaa kuwa rafiki, na vipi inapelekea watu waishi kwa furaha,upendo na udugu kama ndugu wa familia moja (udugu wa kidamu).Mwanaadamu mfano wa matope ,hatuwezi kutamka na kuziita hizi ni tope au udongo mkavu isipokuwa baada ya kujishikamanisha na maji .Hebu tuangalie mfano wa majengo tunayoyajenga sisi wanadamu tunayajenga kutokana na vitu shikamanishi ,vilivyochanganywa mathalani tupige jicho la kiusomi tutakuta ndani yake kuna Mchanga au udongo ,maji ,saruji au
simenti,nondo,miti ,mabati au makuti N.k.Hebu tutafakari tena kwa jicho pekuzi tuutupie jicho kwa mara nyengine Mnazi na mifano ya miti mingine Mnazi ni mjiti wenye mizizi membamba ambapo vidole vya mwanaadamu vipana lakini mizizi hayo yameshikana vyema na kuufanya mnazi ukanawira kwa namna iliyo mzuri yenye kuvuta sayari ya mwanaadamu kupitia kiongo chake cha macho;mnazi unanawiri vyema iwe katika ardhi ya mchanga au udongo.Haya na mifano mengine ni taswira faafu inayotufafanulia maana na umuhimu wa urafiki . Binaadamu ni kiumbe ambae maisha yake yanatekemea msaada kutoka kwa watu wengine ,mbora yetu ni Yule ambae anaejifunza kujuwa namna ya kukaa na watu vizuri.Mwanaadamu popote alipoanahitaji kuwa na marafiki ,na rafiki bora ni Yule mwenye kujishikamanisha na khulka iliyomzuri.Hebu tujiulize khulka mzuri ni ipi? Fasili ya khulka katika Kiswahili inamaana tabia au nyenendo zinawezekana kuwa ni mzuri au mbaya .Mwanaadamu bora ni Yule ambae atakayejishughulisha na khulka iliyomzuri inayoridhiwa na uislam .khulka mzuri ni ambao inayokwenda sambamba na maadili na tamaduni za jamii Neno Maadili limefafanuliwa vyema kupitia mtandao wa Wikipedia inasema ‘’Maadili ni mafundisho yanayotolewa katika nafasi mbalimbali, hasa katika malezi, ili kuelekeza binadamu atende namna ambayo inamjenga yeye na jamii nzima.Maadili yanayohitajiwa na watu wote kimsingi ni yaleyale, lakini mazingira yanaweza kudai yatekelezwe kwa namna tofauti kiasi.Pamoja na hayo, watu tangu zamani wametoa maadili namna maalumu kulingana na dini, utamaduni, falsafa n.k’’. (http://sw.wikipedia.org/wiki/Maadili/08.01.2014/03:24/) tuinaomba tufahamike vyema hapa hatuna maana yakwamba ubinaadamu mzuri ni ule wenye kushikamana na maadili na tamaduni zetu sisi wanajamii la lahsha ,bali tamaduni na maadili tunazozitilia mkazo hapa ni zile zilizo mzuri zinazoendana na mishipa na damu zetu za kiislamu. Fasiri ya Ubinaadamu ni tafsiri ya urafiki ,hapa tuna maana kwamba urafiki sio kitu cha muda mfupi isipokuwa ni dhana inayodumu miaka kenda ,kenda kenda.Hapa huwenda tukajifunza mengi katika maisha yetu sisi wanadamu,awali tunapata kujuwa Watu wasiodumisha urafiki wao huwenda wamekosa khulka iliyomzuri,neno Khulka limeshajumuisha mambomengi ; yote yakiwemo upendo,utu,umoja ,ukinaifu,udugu,ihsani,huruma,imani,uaminifu, n.k.Kwa nini urafiki wetu usiwe ni wenye kudumu ? tatizo liko wapi na vipi tufanye ilimradi tuijenge jamii iliyomoja .Urafiki mzuri ni kama vazi ,kuitwa kanzu ,shati au suruali kumepatikana baada ya kuunganishwa kwa vipande vidogovidogo vya nguo vilivyounganishiwa na nyuzi mbalimbali hata ikapelekea kuwa na vazi lenye kuvutia . Mwanaadamu mzuri mwenye kujielewa lazima kila anapotembea huhitaji kuwa na marafiki waliowazuri ili siku ya nyingine asiwe mgeni wa mji huo .Tujiulize ni wasomi wangapi wanojiunga na vyuo totauti hapa Tanzania na nje ya Tanzania utawakuta baadhi ya watu wanamaliza katika ngazi ya cheti,stashahada au ngazi ya shahada hata bila ya kuwa na rafiki wa ukweli .Unamkuta mtu anaishi maisha kuvikariri vitini bila ya hata kuipa nafasi taswira hii ya Ubinaadamu na urafiki .Mafanikio yoyote katika maisha yanategemea juhudi zetu sisi wanadamu zikichangiwa kwa asilimia kubwa zaidi juu ya mwegemo huu wa urafiki.Palipo urafikia ndipo palipo na adili ya heshima .Dhana ya heshima ianjifafanuwa vizuri katika shairi lifutalo:- 1. Leo yameshatugusa, kuyaeleza twaweza Yanayoharibu hasa, na heshima kupoteza Heshima umeutosa, ulimwenu unacheza Ulimwengu wa makosa, Watu ulowapendeza 2. Heshima imehashama, Si mkumbwa si modgo Watu wanenda marma, Mambo ni giritivyogo Wameyaacha ya nyuma, na kuwekea sokigo Sokigokimesimama, Sasa heshima ni ndogo 3. Heshima ni kama ndoto, ya kuokotea dola Kuzipata ni fikito, na miaka mia lala Itakuwa sokomoto, huzipati kwa hafla Hafla heshima moto, yaunguza kwa ujumla 4. Leo huioni heshima, popote unapoenda Fano la kile kisima, Asali kinachounda Mwana hamtii mama, ulimwengu umepinda Umepinda kwa heshima, kila kitu cha yoyoma 5. Kila kitu cha yoyoma, Urafiki umekwisha Chokochoko zisimama, Na ugomvi usokwisha Khulka zimeangama, Muangamo wa kutisha Urafiki na hekima, heshima elimu tosha 6. Heshima ungelirudi, Pasingekuwa maovu Watu wakawa jadidi, Kuzondoa zote kovu Heshima ungelibidi, Kuuzika uchakavu Uchakavu ni hasidi, heshima kukosa nguvu 7. Lau ningelikuona, popote pale ulipo Maneno ningelinena, na kukurai uwepo Heshima ningekubana, ubakie papo hapo Papo hapo wewe mwana, heshima ungekuwepo 8. Nani alo na heshima, anambiye tumfate tuutowe wote wema, na heshima tumpate Aujenge wetu uma, usipate meza mate Mate yawe kama hema, kwetu heshima tulete. (shairi la Heshima,mtunzi MOH’D ,MOH’D S. katika kitabu cha Gombe la udongo (hakijachapishwa) Napenda nieleweke vizuri hapa ,mshairi hakuwa na maana ya kuwa watu wote hawana hehima ya kuwa heshimu wakubwa kwa wadogo na wadogo kwa wakubwa ,bali mshairi mantki yake ni kuwahamasisha wanajamii hao waachane na tabia mbovu zinazopelekea kupungua au hata kukosekana kwa heshima kabisa .Na vilevile kuwasisitiza hawa hawa washikamane na nyendo nzuri wanazozionesha wakiwa na wamekaa na wadogo zao au hata wanapokuwa na wakubwa zao ,hali hii hupelekea kuimarisha heshima ndani ya jamii.Napenda niwaweke sawa wasomaji wa makala hii urafiki na ubinaadamu hautakuwa mzuri kama hapatakuwa na dhana mzima hii ya heshima.Bado tunatilia mkazo kwayo tungalipo kunako msingi uleule wa mada yetu kuu ya Urafiki na ubinaadamu.tukiendelea zaidi ,tunapoheshimiana hakika hapatakuwa na kovu au aina yoyote ya kuuvunja urafiki na udugu.Mathalani tufikirieni Mababu wetu wa kale ambao waliozaa Wazazi wetu hata kukapatikana ‘’ Mjukuu,Kituu, Kilembwe,Kilembwekeza hadi Kinying’inya’’Mohammed,S.A,(2007) Wao walikuwa wakiheshimiana na kuthaminiana hata ikafikia watu katika mtaa au kijiji wakiishi kam ni ndugu wa damu moja waliotoka tumbo moja .Walikuwa mithili ya kamba inavyoshikama hata kama inatokana na kitu dhaifu usuli wake kwa mfano baadhi ya kamba zinatokana na usumba au masuwe au masumba ya kumbi la mnazi ,kamba nyengine zinatokana na nyuzi za kiroba au kipolo ,na hata nyengine inasemekana zinatokana na Mwani – zao mion goni mwa mazao yanaopatikana baharini.Hii ni mifano ya nmna watu walivyokuwa.Ingawa walikuwa dhaifu kihali na kimali inavyosemekana lakini bado Ubinaadamu na urafiki bado ilikuwa ni nguzo imara kwao wao si katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wala si Katika miezi mengine.Waliishi kwa kujaliana na kuhurumiana katika harakati zao zote.Sambamba na hilo,hata kama inasemwa walikosa elimu hii ya kidunia lakini hakika walikuwa na hekima na busara ya hali ya juu.Walikuwa na ndimi za mawasiliano,wanajuwa namna vya kuwaliana wao kwa wao na hata kwa wenziwao.Walikuwa na upendo wa kusaidiana katika shida na furaha mathalani katika misiba ,harusi n.k.Licha ya kwamba hakuana mwanadamu alikuwa mkamilifu wa asilimia mia moja ,anaweza akawa na kasoro;nao hawa walikuwa na kasoro zao kama ni sehemu za mwanaadamu wa kawaida .kasoro za mwanadam yoyote aliopo au asiopo duniani ni njia moja katika kuimarisha Ubinaadamu na urafiki kwasababu Binaadamu hujifunza kutokana na makosa yake yeye binafsi yake au hata ya mwenzake. Mfano mwengine wa kujifunza panapokuwa na ubinaadamu na urafiki inakuwa ni sawa na mbao zilizounganishwa kwa misumari na kukalafatiwa (kukalafatiwa inamaana kuingizwa sehemu ya mbao zilizo wazi ili kuzuia maji yasivuje au yasipenye) kwa pamba na kutengeneza umbo la Mashua au Jahazi likamvuusha na kumsafirisha binaadamu huyu huyu kwa amani na furaha kutoka kisiwa kimoja kwenda kisiwa kingine.Huu ni mfano ule ule wa ubinaadamu na urafiki ,panapo mashikamano ndipo palipo na hazina na kipuli hiki cha Ubinaadamu na urafiki. Mwisho, katika makala hii tumekusudia kuhamasishama kuwa na ubinaadamu unaoendana na urafiki,makala hii tunatarajia itakuwa ni muwamsho wa hisia za watu zitazowafanya wawe na marafiki wa aina kwa aina ili msomi hata asiyekuwa msomi tunatarajia hatakuwa mgeni mbele ya macho ya watu .Hii huwenda ikawahamasisha hata wasiokuwa waislam wakahamasika na uislam wakasilimu kwa nia safi nyoyoni pasi na kutumia mabavu .kama wanavyosema waswahili maneno mazuri ni hikma kwa mwanaadamu mwenzako.Tunajifunza yakwamba ndege hunasa kwa urimbo uliomwepesi sana usioganda katika meno ya mtu ,lakini unaganda katika miguu ya ndege akatuama hapo hapo kama ulivyo, unavyo na utakavyotuama Ubainaadamu na urafiki.Ni wangapi wanaojuwa kujuwa wakaweza kujuwa.Ni wangapi wanaopata neno wakalishika neno bila ya kuleta neno lisilo neno.Ni wangapi wanaojuwa maana ya maana katika maana ya maana.Huu sio makala ya wakati wa kuendesha baisikeli baharini badala ya kuitembeza barabarani. Wala sio ya kuzirusha Gari angani kwa kutumia marobani mahiri katika anga tulivu badala ya kuzitembeza barabarani kadhalika.Wala ndege kunyonyoka mbawa sio mwisho wa kuruka katika mawingu ya ubinaadamu na uarafiki.Tunatarajiwa makala hii itakuwa kumbukumbu kubwa kwa watu waliotangulia mbele ya haki,tuliopo duniani na wale wataokuja duniani(watakao zaliwa).Ubinaadamu na urafiki unapaliliwa na mboleya ya samadi inaotokana na burasa,upendo,udugu,utu,khulka njema ,heshima n.k. zilizochanganywa kwa pamoja.Mboleya hii inapoingizwa katika ardhi huifanya ardhi hiyo yote iwe na rutba nzuri sana ya hali ya juu.Ardhi hiyo unapoupanda mti wowote humegeka na kubadili umbo ,ambapo mizizi inakuwa inakuwa iko juu angani wakati matunda yake huwapo chini ardhini.Matunda haya huwa yanajimenya wenye na kujimenya wenyewe na kuyanya kila macho yanayoyaona yashuhudie ukweli huu.Kwavyo ukaitwa kwa jina la Mti Ubinaadamu na upendo.Urafiki na ubinaadam ni sawa na kidole kimoja kisivyoweza kubanja chawa .Mfano hata kisivyoweza kuseti nywele kichwani.Jamii zinapaswa zinadilike ziishi kwa kutegemeana na kusaidiana katika maisha.Tatizo kubwa lililopo saa hivi ,Watu wameusahau usemi usemao ‘’Rafiki wa kweli utamjuwa wakati wa dhiki’’Binaadamu wa leo huomba mwenzake akumbane na tatizo kisha amcheke,Urafiki wa kale wa watu wa kale uliacha historia na wamekuwa ni kigenzo chema kwetu sisi.Kwanini sisi hatuna Urafiki na ubinaadamu wa kweli tena wa kudumu? Watu wamekosa mashirikiano katika malezi ya watoto na hata wanafunzi wetu katika shule zetu kinyume na walivyokuwa wababu zetu, ambapo hili lilihamasisha ubinaadamu na uarafiki.Zamani inasemwa Mtoto akifanya kosa iwe shuleni au mtaani liwe kosa la aina yoyote anaadhibiwa na Mzee yoyote na pindipo mtoto huyu atakapodai kwenda kusema kwa wazazi/walezi wake na huko pia huengezwa adhabu nyengine.Hawa walikuwa ni wenye kuifanyia kazi dhana ya uwajibikaji ,walikuwa kila jambo wakilivalisha vazi la hekma na busara hata wakausawiri vyema Ubinaadamu na urafiki na nmna mzuri ya kujuwa kukaa na watu ,pia walijuwa namna na misingi ya ukarimu na kumkaribisha mgeni .Mgeni aliunga urafiki na urafiki ukamalizia udugu. Malengo ya makala hii itusadie hapa tulipo,tunapoishi na wale watakaoishi katika vituo vyao vya kazi waishi vizuri na wenziwao katika hali ya ubinaadamu na Urafiki wa hali ya juu.Na tunakusudia iwe kirekebisho cha Jamii /Watu binafsi ambao wanaishi pasi na kuijali Taswira hii ya Ubinaadamu na Urafiki.

No comments:
Post a Comment